Sura ya 88 katika Msahafu, aya 26, inaanzia ukurasa wa 592.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Je, imekufikia habari ya Msiba wa kufudikiza?
2. Siku hiyo nyuso zitainama.
3. Zikifanya kazi, nazo taabani.
4. Ziingie katika Moto unaowaka.
5. Zikinyweshwa kutoka chemchemi inayochemka.
6. Hawatakuwa na chakula isipokuwa kichungu chenye miba.
7. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
8. Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
9. Zitakuwa radhi kwa juhudi yao.
10. Katika Bustani ya juu.
11. Hawatasikia humo upuuzi.
12. Humo imo chemchemi inayomiminika.
13. Humo vimo viti vilivyonyanyuliwa.
14. Na bilauri zilizopangwa.
15. Na matakia safu safu.
16. Na mazulia yaliyotandikwa.
17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyoumbwa?
18. Na mbingu jinsi ilivyoinuliwa?
19. Na milima jinsi ilivyowekwa imara?
20. Na ardhi jinsi ilivyotandazwa?
21. Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
22. Wewe si mwenye kuwatawalia.
23. Lakini anayerudi nyuma na kukataa.
24. Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
25. Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
26. Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.