Nembo ya TartilTartilRedio mubashara

Sura Al-A'la: maandishi na tafsiri ya maana

Sura ya 87 katika Msahafu, aya 19, inaanzia ukurasa wa 591.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura At-TariqSura Al-Ghashiyah ›

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

1. Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa.

2. Aliyeumba, na akaweka sawa.

3. Na ambaye amekadiria na akaongoa.

4. Na aliyeotesha malisho.

5. Kisha akayafanya makavu, meusi.

6. Tutakusomesha wala hutasahau.

7. Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhahiri na yaliyofichikana.

8. Na tutakusahilishia yawe mepesi.

9. Basi kumbusha, kama makumbusho yanafaa.

10. Atakumbuka mwenye kuogopa.

11. Na atajitenga mbali nayo mpotovu.

12. Ambaye atauingia Moto mkubwa.

13. Tena humo hatakufa wala hawi hai.

14. Hakika amekwisha fanikiwa aliyejitakasa.

15. Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.

16. Lakini nyinyi mnapendelea maisha ya dunia!

17. Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.

18. Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo.

19. Vitabu vya Ibrahimu na Musa.

Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)

Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura At-TariqSura Al-Ghashiyah ›