Sura ya 90 katika Msahafu, aya 20, inaanzia ukurasa wa 594.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Ninaapa kwa Mji huu!
2. Nawe unaukaa Mji huu.
3. Na ninaapa kwa mzazi na alichokizaa.
4. Hakika tumemuumba mtu katika taabu.
5. Ati anadhani hapana yeyote atakayemuweza?
6. Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
7. Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anayemwona?
8. Kwani hatukumpa macho mawili?
9. Na ulimi, na midomo miwili?
10. Na tukambainishia zote njia mbili?
11. Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
12. Na nini kitakachokujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
13. Kumkomboa mtumwa.
14. Au kumlisha siku ya njaa,
15. Yatima aliye jamaa.
16. Au masikini aliye vumbini.
17. Tena awe miongoni mwa walioamini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
18. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.
19. Lakini waliozikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
20. Juu yao utakuwa Moto uliofungiwa kila upande.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.