Sura ya 112 katika Msahafu, aya 4, inaanzia ukurasa wa 604.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa Pekee.
2. Mwenyezi Mungu ndiye Mkusudiwa.
3. Hakuzaa wala hakuzaliwa.
4. Wala hana anayelingana naye hata mmoja.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.