Sura ya 102 katika Msahafu, aya 8, inaanzia ukurasa wa 600.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Kumekushughulisheni kutafuta wingi.
2. Mpaka mkaja makaburini!
3. Sivyo hivyo! Mtakujajua!
4. Tena sivyo hivyo! Mtakujajua!
5. Sivyo hivyo! Lau mngelijua kwa elimu ya yakini.
6. Basi bila ya shaka mtaiona Jahiimu!
7. Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
8. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema zote.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.