Sura ya 101 katika Msahafu, aya 11, inaanzia ukurasa wa 600.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Inayogonga!
2. Ni nini inayogonga?
3. Na ni nini kitachokujulisha ni nini inayogonga?
4. Siku ambayo watu watakuwa kama nondo waliotawanywa;
5. Na milima itakuwa kama sufu zilizochambuliwa!
6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito.
7. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
8. Na yule ambaye mizani zake zitakuwa hafifu.
9. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
10. Na ni nini kitachokujulisha ni nini hiyo?
11. Ni Moto mkali!
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.