Sura ya 92 katika Msahafu, aya 21, inaanzia ukurasa wa 595.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Ninaapa kwa usiku unapofunika!
2. Na mchana unapodhihiri!
3. Na kwa aliyeumba dume na jike!
4. Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
5. Ama mwenye kutoa na akamcha Mungu.
6. Na akalisadiki lililo jema.
7. Tutamrahisishia yawe mepesi.
8. Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake.
9. Na akakanusha lililo jema.
10. Tutamrahisishia yawe mazito!
11. Na mali yake itamfaa nini atakapokuwa anadidimia?
12. Hakika ni juu yetu kuonyesha uongofu.
13. Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
14. Basi nakuonyeni kutokana na Moto unaowaka vikali.
15. Hatauingia ila mwovu kabisa!
16. Anayekadhibisha na akageuka na kwenda zake.
17. Na mcha Mungu ataepushwa nao.
18. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
19. Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndiyo anamlipa.
20. Ila ni kutaka uso wa Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
21. Naye atakujaridhia!
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.