Nembo ya TartilTartilRedio mubashara

Sura Ad-Duha: maandishi na tafsiri ya maana

Sura ya 93 katika Msahafu, aya 11, inaanzia ukurasa wa 596.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Al-LailSura Ash-Sharh ›

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

1. Ninaapa kwa wakati wa kabla ya adhuhuri!

2. Na kwa usiku unapotanda!

3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.

4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko uliotangulia.

5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.

6. Kwani hakukukuta yatima, akakupa makazi?

7. Na akakukuta umepotea, akakuongoa?

8. Akakukuta mhitaji akakutosheleza?

9. Basi yatima usimwonee!

10. Na anayeomba au kuuliza usimkaripie!

11. Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie.

Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)

Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.

Sikiliza visomo vyakeSoma sura hii katika Msahafu pamoja na tafsir‹ Sura Al-LailSura Ash-Sharh ›