Sura ya 94 katika Msahafu, aya 8, inaanzia ukurasa wa 596.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Hatukukunjulia kifua chako?
2. Na tukakuondolea mzigo wako.
3. Uliovunja mgongo wako?
4. Na tukakunyanyulia utajo wako?
5. Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi.
6. Hakika pamoja na uzito upo wepesi.
7. Na ukipata faragha, fanya juhudi.
8. Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.