Sura ya 97 katika Msahafu, aya 5, inaanzia ukurasa wa 598.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur-ani katika Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu).
2. Na nini kitachokujulisha nini Laylatul Qadri?
3. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
4. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.
5. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.