Sura ya 107 katika Msahafu, aya 7, inaanzia ukurasa wa 602.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
1. Je, umemwona anayekadhibisha Malipo?
2. Basi huyo ndiye anayemsukuma yatima.
3. Wala hahimizi kumlisha masikini.
4. Basi, ole wao wanaoswali.
5. Ambao wanapuuza Swala zao.
6. Ambao wanajionyesha.
7. Na wanazuia msaada.
Tafsiri ya maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center, toleo la 1.0.5, imechapishwa bila mabadiliko kutoka QuranEnc.com. (QuranEnc.com)
Tafsiri huwasilisha maana za Qur'ani tu; si Qur'ani yenyewe. Qur'ani ni maandishi ya Kiarabu yaliyo hapo juu.